`MAFUNDISHO YA WAAMINI WAPYA
SOMO 1 BIBLIA Kuelewa Biblia .
Utangulizi:-
Neno la mungu.”Biblia Takatifu”.Nikitabu Maalum cha Mungu.) Ikiwa na maana Biblia =>Kiswahili chake kitabu.)
Kiliandikwa na watu wengi tofauti na kiliandikwa kwa kiongozwa na Roho mtakatifu. 2Timotheo 3:16.
Biblia ni moja wapo ya vitabu vya zamani sana ulimwenguni. Sehemu za zamani kuliko zote za Biblia ziliandikwa karibu miaka 4,000 iliyopita. Katika hiki kitabu tunapata majibu makubwa maishani.
(1)Ninatoka wapi?
(2)Kwanini? Niko hapa?
(3)Ninakwenda wapi?
Biblia ina vitabu 66 vinavyopatikana katika orodha yake na imegawanyika katika makundi mawili (1)Agano la kale.(2)Agano jipya.
Agano la kale: linatuambia kuhusu kazi ya mungu na watu wake kabla ya kuzaliwa kwa yesu,maisha yake, huduma yake ya kuponya wagonjwa na kusamehe kwenye dhambi, Kifo chake msalabani,kufufuka kwake katika wafu na kupaa kwake.
Neno “Agano”:Maana yake ni Patano” Agano la kale ni patano ambalo mungu alipatana na mtu kuhusu wokovu wake kabla yesu kristo hajaja. Agano jipya ni patano ambalo mungu alipatana na mtu kuhusu wokovu wake baada ya yesu kristo kuja.
Nguzo ya Biblia
Biblia ni maandiko kuhusu historia ya mungu kuwaokoa watu ambao wameaanguka katika zambi.
(1)Mungu aliumba ulimwengu na binadamu(mwa 1:-2:)
(2)Binadamu alimuasi mungu kwa kutomuamini na akaanguka(mwan3:1-20)
(3)Mungu alimuita iblahimu ilikuwaonyesha njia ambayo walianguka toka kwa mungu mwenyewe (mwa 12:1-3)
(4)Mungu aliweka Agana na Islaeli na kuwaambia katika historia yao.
(5)Mungu aliturudisha kwake mwenyewe kwa njia ya Yesu kristo na kutimiza wokovu kwa njia ya msalaba.(Injili 4:mt Molkyn)
(6)Mungu anatangaza neon lake kwa njia ya kanisa na kuenderea kufanya kazi ya wokovu mdo.1:-28)
(7)Kurudi kwa Yesu kristo na siku ya mwisho ya hukumu.
(8)Nchi ya mungu iliyokamilika uf. 1:22:-)
NINI KIINI CHA BIBLIA
Yesu kristo ndiye kiini cha biblia Yoha 3:16 “Yaliyomo katika biblia”
(1)Inaonyesha ukweli huu:
Binadamu ulijaribiwa na shetani,binadamu atakwenda jehanamu ya moto kwasababu ya dhambi hiyo(mwa 3:1-15;Ef 261-3)
(2)Niahadi kuwa walikuwa wakimuamini Yesu kristo ambaye ni masihi aliyekuja kwa binadamu ambao wako katika dhambi,wataokolewa (mwanzo 3:15)
(3)Ushahidi ni Agano jipya kwamba masihi ambaye ameahidiwa zaidi ya mara mia nne.Katika Agano la kale amekuja ulimwenguni . Isaya 7:14 mat1:21
=>Biblia imetabili kurudi kwa bwana Yesu mara ya pili mara 15,000:
Niahadi kwamba mtu ambaye anampokea Yesu kristo huyu Roho mtakatifu anakaa ndani yake na kumwongoza (yoh 14:16; 26:Rom8:2)
TABIA YA BIBLIA:
(1)Biblia ni neon la mungu.
2Timo3:15-16
.Linaleta uzima .yoh 6:63.
.Nila umbaji Zaburi33:6,9, Ebran 11:3
.Nimaji (au) kama maji yohana15:3 Efeso 5:25-27.
.Hututunza kwa usafi. Zab 119,9,11
.Nitaa ya maisha yetu 2 Petro 1:19
.Linatupa ufahamu katika ulimwengu wa giza Zab19:8 Zab119:105,130
.Nichakula cha kiroho mt 4:4
.Linasababisha kukua kiroho Ikor3:1-2 . 1Petr 2:2 .Efe4:12-13
.Nimbegu Luka 8:14-15 Ilituzae matunda Zab1:3 .2kor9:10
.Niupanga Efeso 6:17. Luka 4:1-14
.Linatusaidia kuomba Yoh 15:7
.Linatutia nguvu ndani yetu mt 7:24-25,26,27
.Nimoto wao ninyundo Yer 23:29
(2)Biblia ni maandiko ya unabii ufu1:3
=>Kama tusipojua neon hili tutahukumiwa kwa sababu imetoa unabii kwa usahihi kuhusu mambo yatayotokea.
(3)Biblia ni ahadi ya milele na itatimizwa kwa kweli katika ulimwengu huu (Isaya 40:8, Mat 5:17-18) Ahadi ya mungu; Biblia haina uongo na nia ya milele kwa sababu mungu ni wa milele.
(a)Jinsi Biblia ilivyoletwa kwetu 2petro 1:21
(b)Ukuu wa Biblia (1kor2:13)
(4)Mtu yeyote hawezi kuondoa neon lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki(Rumb.4:2; ufu22:18-19). Biblia nineno ambalo linawaongoza watu kwa njia ya nuru na kuwaimarisha kwa nguvu (zab 19:7-14,119:105).
(5)Biblia ni silaha ya kufahamu mapenzi ya mungu na kushinda nguvu za shetani.
(6)Nikitabu kinachoweka hila za shetani wazi(mw 3:1-29 Ef 6:10-20,Yoh8:44 Yoh3:8; Uf 20:2,10 Yako4:4 Lk10:18)
SOMA 2
MUNGU
Mungu ni Roho. Yoh4:24,mw1:2. Yeye ni mkuu mno kwetu sisi kumfahamu kwa wazi. Hana mwanzo wala mwisho. Hakuna sehemu ambayo uwepo wake hauonekani. Biblia inatueleza katika kitabu cha Ayubu 11:7
Mungu anaishi mbinguni na anatawala ulimwengu wote Biblia inatuambia Isaya 66:1 Zab 47:8)

MUNGU NI WA NAMNA GANI:
(1)Mungu ni muumbaji wa vyote Nehe 9:6) Zaburi 139:13
(2)Mungu ni mwenye nguvu zote Rumi 9:19-21 1Nyak 29:11 Efeso 3:20
(3)Mungu anajua yote.Ebr 4:13 1Yohana 3:20
(4)Mungu ni Mtakatifu 1Samweli2:2
(5)Mungu ni moto ulao. Ebrania 12:29 Torati 4:24 Isaya 33:14.
(6)Tunaweza kumjua mungu wako 4:8 Zaburi 145:18
(7)Mungu ni baba wa upendo 1Yohana3:1
MUNGU NI MKUU MNO
KUISHI KWENYE MAHEKALU
.Mdo17:24-25,28
MUNGU WETU NI MMOJA
.Torati 6:4-5
AMEJIDHIHILISHA KATIKA NAFSI TATU
Mwanzo1:26. Mwanzo3:22-23. Mwanzo 11:7
NINANI JINA LA MWANAE
Methali 30:3-5. Maandiko yanamzungumzia Yesu atakaekuja na kupaa.
.Nafsi tatu zajifunua wazi wakati wa ubatizo Mathayo 3:16,7.Yesu,Roho,sauti ya baba mungu.Mathayo 28:19 Agizo la YESU.
Kwajina la baba,mwana,Roho. Duniani wapo watatu
1Yohana5:6,5:9
Watu washuhudia mbinguni 1Yohana5:8
Hivi ndivyo mungu alivyojifunua.
HALI ZETU MBELE ZA MUNGU
Jinsi tulivyo mbele za mungu
(1)Tumeumbwa na mungu Zaburi 139:14-16
(2)Sisi ni mali ya mungu 1kor6:19-20
(3)Tumeitwa kumuabudu mungu Uf 4:11
Agizo la yesu ni kumpenda mungu.Math 22:37) fanya uchunguzi sahihi Yoshua 24:15
Soma 3. Binadamu na shetani
(A)Mtu-sura ya mungu aliumbwa awe na mamlaka.
Mungu alikuwa na kusudi kamili la kumwomba mwanadamu(me/ke)
Kwasababu mungu ni upendo alitaka kuwa na viumbe vya kufanananaye kiakili na kwamoyo,watu ambao nao angeweza kushirikisha maisha yake yote yeye alivyo na yote anayoyafanya watu ambao watatawala mbingu na inchi pamoja naye kama wana.
Aliumba mtu katika mfano wake mwan1:26-27
(B)LUSIFA
Mungu aliumba vitu vingi vya ajabu kabla ya kuumba mbingu na Inchi kati ya hivyo walikuwepo malaika-viumbe.Vya kiroho kusudi lake ni kufanya mapenzi ya mungu-Malaika humuabudu mungu na kumtumikia kwakudumu: Ufu5:11-14
Hata ikiwa lusifa mmojawapo wa malaika wakuu;alimwasi mungu alitaka kuwa juu ya kiti cha enzi cha mungu.
Badopia alitaka utawala ambao mungu alimpa mwanadamu baada ya kuumba dunia.
Wakati lusifa alipoasi, mungu alimfukuza mbinguni.
Theluthi moja ya malaika waliungana naye katika uasi wake,nao pia wakafukuzwa pamoja na lusifa (Uf 12:4) Isaya 14:12-14
Alitupwa duniani ambako leo anajulikana kuwa ni shetani au Ibilisi Ezekieli 28:11-17.amekuwa muovu na kujawa na giza.
Baada ya kutupwa bado alianza kupanga mipango mingine ya kuchukua utawala wa duniani kwa kumshambulia mtu.Yule ambaye mungu alimuumba na kumpa utawala wadunia.
Majaribu kati ya shetani na mwanadamu mwanzo2:9,17 Ebr2:8 Mwanzo 2:15-17. Shetani alimdanganya Hawa,mwanzo3:6. 1Timotheo 2:14.
Hawa aliamini uongo huo na akala tunda la mti huo .Adamu ingawa naye alijua kuwa huo ni uongo pia naye alikula
MATOKEO
Kwatendo hilo moja la dhambi; mwanadamu alipoteza utukufu na sura ya mungu na mamlaka juu ya uumbaji.
Kisha shetani alichukua nafasi iliyoachwa na Adamu na Hawa na akaanza utawala wake juu ya Inchi na ndipo mauti ilipoujaza ulimwengu.(Ebr2:14-15)Rumi 5:12)
Kwahiyo vizazi vyote vilivyomfuata Adamu na Hawa vimerithi asili yao ya dhambi na uasi.Vyote vimekuwa chini ya nguvu za utawala wa shetani Efeso 2:1-3.
Mioyo ya watu sasa kila mahali,sasa imejawa na (1)kuabudu
(1)Sanamu. Rumi1:21-23
(2)Uchafu:Rumi1:24-27,
(3)Aina zote za uovu: Rumi 1:28-32.
SOMO 4
YESU:
Yesu ni mwana wa mungu:
Luka1:26-35
Bikira alichukua mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu akamzaa yesu,Alikuwa ni mungu mwenyewe aliyekuja duniani kwanamna ya kibinadamu.Aliye juu luka1:26-35.yh1:1,14
Alikuja ulimwenguni kwa kusudi maalum.
(1)Kumkomboa mwanadamu kutokana na nguvu za shetani. Luk19:10, kolo1:13
(2)Kutoa uhai wake kama fidia kutununua tena.(mt 20:28)
(3)Kuzivunja kazi za shetani katika maisha yetu: (1yoh3:8)
(4)Kutupa sisi uzima wa milele 1yohana5:11-12. Yoh3:16-17.yohana10:10
(5)Kutupa sisi”kuzaliwa” upya na kuungana na familia ya mingu.Yh1:12)Angalia 1yohana3:1-2
(6)Kurejesha ushirikiano wetu na mungu Baba.(1yohana1:3)
Yesu alikuja kutuonyesha vile mungu anavyofanana:yh14:7-11.Yohana1:18.
(1)Alituonyesha upendo wa mungu 1Yohana4:9-10, Runi5:8
(2)Alituonyesha nguvu za mungu .
Aliponya wagonjwa,viwete na vipofu.Mt 4:24 Yohana 9:1-7
Alitoa pepo wachafu: Mk1:34 Marko5:1-7
Alifanya miujiza (Mk 4:37-41) Yoh6:1-2
Alifufua watu.Yh 11:43-44)
YESU ALISHIRIKI MATESO YETU KATIKA MAISHA YAKE
Yesu alishiriki matatizo yote tunayopitia hapa duniani Ebr 4:15,math 8:17
Yesu alikufa msalabani kwa ajili yetu (Mark 15:16-39. 1petro2:24, Isaya 53:5-6.
Yesu alifufuka kutoka wafu kwa ajili yetu.Mathayo28 Efeso 2:4-6 Waruni 6:4
=>Yesu alifungua mlango wa mbingu ni kwaajili yetu Ebr 10:19-22.Yohana 14:1-3
SOMO 5 “Msalaba”
Waliomtesa yesu hawakutambua kwamba msalaba ulikua umepangwa na mungu tangu misingi ya ulimwengu.
(A)Mungu hushughulikia dhambi zote.
Yesu alikuwa anakufa mahali pakila mtu katika ulimwengu.Kupokea binafsi kile alichofanya msalabani huleta jibu binafsi kile alichokifanya msalabani huleta jibu la mahitaji yetu yote.
Mungu hufunua nguvu zake kwa njia ya msalaba 1kor1:18 Rum1:16
Mungu huonyesha upendo wake pale msalabani Rumi5:8.
Mungu aliondoa huzuni zetu pale msalabani Isaya 53:4
Yesu alichukua adhabu ya dhambi zetu pale msalabani. Isaya 53:5-6 1petro2:24
UHUSIANO MPYA NA MUNGU KWA NJIA YA MSALABA:
Kwahiyo kwa kufa msalabani siyotu kwamba Yesu aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu mahalin petu bali pia alifanya iwezekane kwetu sisi binafsi kumjua mungu na kukutana na upendo,amani na furaha ambayo huletwa na ushirika pamoja naye.
Tunakubalika kwa mungu kwa njia ya msalaba 2kor 5:21
Tunapata msamaha wa Dhambi kwa njia ya msalaba 1:13-14 ,1Yoh2:1-2
Tunakuwa washiriki wa familia ya mungu kwa njia ya msalaba Ebr2:11-12 Yohana 1:12
Vizuizi vya kitaifa vinavunjwa kwa njia ya msalaba. Efeso2:13-16
UHURU KWA NJIA YA MSALABA.

Msalaba umetupatia uhuru mkumbwa kwa ajili yetu.
Uhuru kutoka kwa shetani kolo2:15 kolo 1:13
Uhuru toka zambi za zamani Yohana 8:36
Uhuru toka zambi za sasa. Rumi6:14
Uhuru toka magonjwa . Mt8:17.
Uhuru toka kana Gala 3:13. Torati 28:15-68
Uhuru toka hukumu. Ebr 9:26-27
Uhuru toka mauti ya milele. Yh 3:16
Upendo na haki Hukutana msalabani Rumi 5:8-11
SOMO 6 DAMU YA KRISTO:
Kumwagika kwa damu ya yesu kristo msalabani kulikua ni muhimu Ilisisi tupate msamaha wa dhambi zetu na kukubaliwa katika uwepo wa mungu Ebr 9:22
Uhai uko katika damu.Law 17:11
Rum 6:23,Yesu alilipa adhabu hii yetu kwa kumwaga damu yake.
Upatanisho unamaanisha kuwa katika umoja na mungu.Yesu alitoa uhai wake(alimwaga damu yake) Msalabani kwa ajili ya upatanisho hivyo ilituwezesha sisi kuwa katika umoja na mungu.Damu ya yesu humaanisha kuwa sisi sio maadui zake tena bali rafiki zake wana wake wakike na wakiume kwa imani tunapokea kile alichokifanya kwaajili yetu.
KILE DHAMBI INACHOFANYA KWA MAISHA YETU
Hututenga sisi na mungu Isaya 59:2
Hutufanya tujione wenye hatia Zaburi 38:4
Humruhusu shetani kutushitaki Ufu 12:10
Hudai Adhabu ya kifo . Ezekieli 18:4
Damu ya kristo hukidhi mahitaji yetu yote.
DAMU NI KWAAJILI YA MUNGU
Damu ya kristo hutosheleza kabisa sheria ya mungu ambayo hutaka adhabu kwa kuvunja sheria 1 Yohana3:4
Damu hutulinda na adhabu (kifo) ya kuvunja sheria.
Katika kitabu cha kutoka 12.Mungu aliwaamuru wana wa Israil kuweka damu ya mwana kondoo kwenye miimo ilikuwalinda na mharibu ambaye angewaulia wazaliwa wa kwanza wote.
Huyu mwana kondoo alikuwa picha ya mwana kondoo yesu ambaye angekuja baadaye.Mungu alisema .Nami nitakapoiyona damu nitapita juu yenu kutoka 12:13
Ushirika unarudishwa. Rumi 5:8-7
=>Tunakombolewa.(Tunanunuliwa upya kutoka utumwani)Efeso1:7
DAMU KWA AJILI YA WATU
Damu imemtoshereza mungu na sasa itutosheleze sisi dhamiri yetu na makosa yetu.
Damu hutusafisha na makosa Ebr 9:14
Damu hututakasa sisi Ebr 13:12
Damu hutuleta karibu na mungu Kolo 1:20-21
Damu hutupa ujasiri wa kuingia kwenye uwepo wa mungu Ebr 10:19-22
Damu hutukamilisha machoni pa mungu Ebr 10:14
DAMU NI KWA AJILI YA IBILISI
Shughuli za shetani za kimbinu mno kwa wakati huu ni kama mshtaki wandugu ufu 12:10. Na ni kwa namna hii Bwana Mwenye hupambana naye katika huduma yake maalum kama kuhani Mkuu kwa njia ya damu yake Ebr 9:11-14
Damu Humweka Mungu upande wa Mwanaadamu kinyume na ibilisi (Rumi 8:31, 33-34)
Ibilisi hanachimbuko la mashitaka dhidi ya wale ambao wapokea tendo la damu ya kristo iliyomwagika kwa ajili yao
Damu Hutengua haki zote za umilikiji wa shetani kisheria kolo 1:14
Ukombozi humaanisha kununuatena? Tuko chini umilikaji mpya, na gharama ambayo ililipwa kwa ajili yetu ilikuwa damu ya Yesu ilimwagika mdo 20:28. (1Kor 6:19-20) (1Timo 2:6)
KILE DAMU YA KRIST0 ILCHOLEYA KWETU:
Usafi wa Moyo, 1 yoh 1:7
Uzima wa Milele, yoh 6:53-54
Kukaribia kwa mungu, Efeso 2:13
SOMO 7
UFUNUO
Baada ya kifo chake pale msalabani Yesu alilala siku tatu Kaburini, mt 12:40 kisha Mungu alimfufua kutoka wafu! “Mathayo 28” rum 1:4.
Mungu Alikufufua wewe pamoja na Kristo. Kifo cha Yesu kulikuwa kwa ajili yako vivyohivyo na ufufuko wake! Efeso 2:1-16, kolosai 13:1-3
Kukupa maisha mapya (2Tim1:9-10)
Kukupa kuzaliwa mara ya pili (1Petr1:3)
Kukupa mwanzo mpya (2Kor 5:17)
Kukupa ushindi juu ya shetani(1Yoh4:4, 5:4,5) kolo 2:13-15
Kukupa Mamlaka juu ya shetani 1Petro 3:21-22) luka 10:17-19
Nguvu juu ya shetani: Ef 1:18-23 Mark 16:15-18 Mdo1:8, 4:33
Kukufanya Mwana na mrithi katika Ufalme wa Mungu, Rumi 8:15-17
UFUFUO HUKIDHI KILA HITAJI LA MAISHA
Niukombozi wako tokea wakati ulipopita., Maisha yako ya zamani ya dhambi yaliwekwa msalabani pamoja na yesu na kuzikwa pamoja naye kaburini. Kisha Yesu alipofufuliwa kwenye uzima tena ulifufuka pamoja naye kama uumbaji mpya ukiacha nyuma maisha yako ya zamani kwenye kaburi la Yesu., Rumi 6:4-11 Efeso 2:1-7 Kolo 2:12-15.
Nguvu yako kwa sasa.
Kwasababu Yesu yuhai tumepata nguvu ya Roho yake ili kuishi Maisha ya ushindi juu ya dhambi na mashambulizi yote ya shetani dhidi yetu., Rumi 8:31-39
Nitumaini lako kwa wakati ujao kufufuka kwa Yesu kuna tupa matumaini makubwa ya wakati ujao. Anaitwa mzaliwa wakwanza. Katika wafu kolo 1:18 na atarudi Duniani tena. 1kor 15:17-23 1kor 15:50-57 1thesal 4:13-18
SOMO LA 8
IMANI

Imani siku zote imekuwa ndiyo alama ya wanafunzi wa Yesu. Wanafunzi wa kwanza walijulikana kama waamini (marko 9:23)
Imani humaanisha kumtegemea Mungukwa hali zote. Wakati Adamu alipofanya dhambi alijitoa katika kumtegemea Mungu na kujitegemea. Hii ndiyo sababu Mungu ameweka kipaumbele cha juu kwenye Imani. Imani ni njia ya kuturudishia uhusiano na Mungu. Kwa hiyo huku kumtegemea Mungu ndo kunaitwa Imani.
Imani inakufungua wewe toka ywezo wenye kiwango. Kwa imani unatoka kwene kutojiweza hadi kujiweza katika uwezo wake. Hii ndiyo njia ya kutembea katika imaniambayo wote tumeitwa. Mt 17:20.
IMANI NI NINI?
Imani ni tendo la uttfu katika kuitikia kile mungu alichosema. Imani ya kweli inaelezewa katika:-
Utii
Tendo lakulingana
Kusikia neon lamungu(sauti) Ebr 11:1
Imani maana yake ni kuwa na tumaini, uhakika au uthibiti kwa mtu mwengine au katika maneno ya mtu Yule. Kuwa na imani kwa mungu huhusisha kubadili kujitumaini mwenyewe na kumtumaini yeye.
Tunaacha kutegemea chanzo cha maarifa yetu yenye ukomo na kuanza kupokea kutoka chanzo chake kisicho na ukomo.
AINA MBILI ZA MAARIFA
1kor 2:4-7, 8-16
Milango ya maarifa.
Naarifa yote yanayokuja kwa mtu wa kawaida yanakuja kwake kwa kupitia milango mitano ya fahamu, kuona, kuskia, kuonja, kunusa, na kugusa, Haya ni maarifa yenye ukomo yaliolezwa kama hekima ya Mwanaadamu.
Maarifa ya ufunuo
Maarifa haya hayweki msingi juu ya milango mitano ya fahamu au kufikiri kwa kawaida lakini juu ya jambo jengineambalo “ni kweli ya neon la mungu” ambayo hupokelewa kupitia roho ya mwaadamu. Na huelezwa kama hekimaya mungu “maana tunaenda kwa Imani si kwa kuona” 1kor 5:7
MSINGI WA IMANI
Asili ya Mungu Ebr 6:13
Hwezi kubadilika, malaki 3”6, ykobo 1:17
Hawezi kushindwa, Ayubu 42:2, 1nyakati 28:20
Hawezi kudanganywa, hesabu 23:19, tito 1:2
Kazi ya ukombozi ya Mwanawamungu Ebr 12:2 Kristo amefanyika chanzo cha imani yetu kwa Mungu. Ukweli kuhusu kifo chake na ufufuko hutoa msingiwa kuamini kwetu. 1kor 1:30
Neno la Mungu
Neon la mungu husimama kweli daima. Imani huja wakati Mungu analeta neon maalumu kutoka yote aliyowahi kusema moja kwa moja kwetukatika hali zetu. Likisemwa namna hii neon la mungu huja kwetu likiwa hailikifungulia imani yetu. Mt 24:35, isaya 40:8 yer 1:12.
JINSI INAVYOTENDA KAZI
Kanuni ya imani sharti hutenda kwa kuendelea katika maisha yetu bila kujali, 2kor 5:7 yakb 1:5:6, Hutenda kwa njia ifuatayo:-
Mungu hutupa imani, warumi 1:7, Habak 2:4. Mwenye haki ataishi kwa Imani yake hiyo ndiyo imani yeye aliyotupa sisi kama kipawa Ef 2:8-9, Rum 12:3
Imani hiyo kwa neno la mungu kwanza mungu anatupa moyo kwa kusema “Neno” linalolingana na hali zetu hii inakuja wakati tunaposoma Biblia au kuskiza sauti ya roho mtakatifu ndani ya roho yake rumi 10:17, mwanzo 15:3-5, 17:15-21, yoshua 1:8
Utii waneno la Mungu
Ili imani itende kazi katika hali zetu ni lazima kutii neno hilo, imani hutenda kazi na siyo tulivu. Ahadi nyingi za mungu zina masharti- atafanya sehemu yake kama tukifanya sehemu yetu. (yak 7:24, 1:22-25 mwanzo 15:6, math 7:24-27).
Shida au majaribu ya imani zenu” hiki ni kipindi cha majaribu. Kila kitu kinachotokea kutuzunguka huonekana tofauti na kile mungu anachosema na hapo huelekea. Hakuna ushindi wa asili wakuamini kwetu. Kwa namna hii imani yetu inakaa katika neno la mungu (kile alichozungumza kwetu) 1Petr 1:6-7, rumi 4:16-21, zab 105:17-19 kwa imani tunajutupa wenyewe katika juu ya uaminifu wake wakati wahofu zetu na mashindano Mungu ni mwaminifu na hatutupi (2timo 2:13) Alikuwa mwaminifu kwa Tomaso na Petro wakati imani yao ilipokuwa iniajaribiwa yesu hawakuwaacha Ebr 13:5.
Matokeo yake
Matokeo ya mwisho siku zote kwa sehemu ya mwamini ni ushindi ikileta utukufu kwa mungu. Yak 1:2-4 mwanz 21:1-3 zabur 105:19-22, mdo 3:16 Ebr 6:13-15 1Yoh 5:4
SOMO LA 9
NEEMA
Kwanini Neema ya mungu ilikuwa muhimu katika uzoefu wa wakristo wa mwanzo kwa nini kanisa Antioka liliomba Neema ya mungu iwe juu ya Paulo na Barnaba na baadae Paulo na Sila walipotoka katika safari zao za umisheni mdo 4:33, 14:26.
Maana ya Neema
Maana ya kawaida ya neno Neema inayofahamika “upendeleo wa mungu ambao hatukustaili”
Kwa maneno mengine ingawa tulikuwa wenye dhambi wenye staili hukumu, mungu alitutazama kwa upendo na akatusamehe,
Pia neema inamaana ya nguvu ya mungu ya kutuwezesha, 2thesa 2:16-17 kwa hiyo sio
Neema yake tu inayotufanya tukubalike katika familia ya mungu lakini pia hutua nguvu tunayohitaji ili kuishi maisha ya kikristo, maandiko mawili yanayo onyesha tabia mbili za neema ya mungu.
Upendeleo wa mungu ambao haukustaili Efeso 2:8-9
Nguvu ya mungu ya kuwezesha, Efeso 1:4-6 katika wokovu sio tuu upendeleo wa mungu usiostahili unaoneshwa (kwamba tunapokea msamaha na kurejeshwa uhusiano nay eye hata kama hatustaili) lakini hivyo pia ni nguvu ya mungu ya kuwezesha kwa vile ni kwa nguvu zake tunaweza kubadilika 2kor 5:17 kanuni hii ya neema inaendelea katika kutembea kwetu na mungu 1Petrn3:18.
NEEMA WALIOWA MASHUJAA WA IMANI
Neema katika maisha ya musa, kutoka 3:11-13, 4:1-13 tukio la musa kutoka kwenye udhaifu na kutojiweza kwake. Mwenyewe lilikuwa kama ifuatavyo:-
3:11 Mimi ni nani?
3:13 Jina lako ni nani?
4:1 Hawataniamini?
4:10 Mimi simsemaji
4:13 Bwana tuma mwingine Lakini kwa neema ya mungu Musa alikwenda misri na kwa ishara ya maajabu wana wa Israeli walitoka kama mungu alivyo mwambia.
Neema katika maisha ya Gideoni Amuzi 6:1-24, Gideoni aliokoa Israeli alifanya hivi akiwa na kundi dogo tu la watu ilikuwa ni neema ndiyo iliyofanya.
Neema katika maisha ya Paulo, mdo 15:40 2kor 11:22-33 inafahamika kwamba aliwekwa kwanza kwa neema ya mungu alihitaji kwa ajili ya kuishi, jibu la Bwana kwa ukiri wa udhaifu wa Paulo ni ahadi yake kwa ajili yetu pia, (2kor 12-9)
Neema iliyofunguliwa kwenye maisha yetu, hii hututhibitishia tuamini vile neno la mungu linachosema licha vile hali inavyoweza kuamini kuonyesha, mwitiko wa Mungu kwa imani zetu ni neema yake. Nguvu yake ya kuwezesha ,ambayo hutusaidia kushinda katika kila hali:
AHADI MBILI MUHIMU
Tunao ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa neema, Ebr 4:16
Mungu kutujaza, 2kor 9:8
SOMO LA KUMI
UBATIZO
Yesu aliamuru wale wote waliomwamini wabatizwe katika maji mt28:18-19, melo2:38-41, “Kubatizwa” maana yake ni kuzamishwa kabisa wakati mtu ametubu dhambi zake na kuamini kuwa Yesu alikufa kwa ajili yake, mbele ya mashahidi wengi, yeye inabidi apelekwe kwente maji awekwe chini ya maji na kutolewa tena.
Kufahamu ubatizo katika maji, kufahamu kile chote ubatizo katika maji unachohusu ni ufunguo wa maisha ya ushindi na ya uhuru ya ukristo.
Tendo la kwenda chini ya maji na kupanda kutoka majini tena ni picha inayodhihirisha kile kilichotokea kwa mwamini wa kristo
SURA YA HATUA NNTE ZA KAZI ZA YA KRISTO.
Alikufa = Nilikufa ndani yake Rum 6:6-7
Alizikwa = Nilizikwa pamoja naye Rum 6:3-4
Alifufuka = Nina maisha mapya ndani yake, Rum 6:4-5
Alipaa = Nilipaa ndani yake Efeso 2:6, kolo 3:1
UBATIZO KATIKA MAJI NI;-
Ibada yako ya mazishi
Ibada yako ya mazishi sio kumuua mtu hufanyika tu wakati mtu ameshakwisha kufa tayari. Na kwa hiyo kwasababu “Umekufa” ndani ya kristo unazika maisha yako ya zamani katika ubatizo ndani ya maji
Ufufuo wako wa maisha mapya
Unapotoka ndani ya maji unaonesha na kutangaza kuwa wewe ni kiumbe kipya katika kristo, Rumi 6:8-11
FALME MBILI
Kila mtu mwanamume na mwanamke anayezaliwa kwenye ulimwengu huxaliwa kwenye ufalme wa giza huzaliwa mtuma wa dikteteta shetani. Hakuna njia ya kutoka katika ufalme huu ispokuwa kwa kifo. Na hakuna njia ya kuingia katika ufalme wa mungu ispokuwa kwa kuzaliwa. Hivyo Yesu alifanyika kwa pamoja kifo chetu na kuzaliwa upya kwetu nah ii ilidhihirishwa katika ubatizo katika maji, kolo 1:13
JAMII MBILI
Kama kulivyo falme mbili ndivyo hivyo kwamba ndani ya kila falme kuna tofauti za jamaa za watu. Jamii ya Adamu ndiyo inayoujaza ufalme wa giza na uumbaji mpya ndio unaoujaza ufalme wa mungu
Adamu wa kwanza
1kor 15:22, rumi 5:12
Adamu alikuwa Baba yetu wote jamii ya Binaadamu. Dhambi ya Adamu ilitufarakisha sisi sote na mungu kwa sababu ya dhambi yake. Sisi sote tuliritki asili yake ya uasi na magonjwa tukafanyika wenye kupasiwa kifo uzao wa Adamu unaitwa “Jamii ya Adamu”
Adamu wa mwisho
hapakuwepo njia ambayo mungu angebadili jamii ya Adamu iliyoanguka. Iliaweke mwisho kwa ile jamii na kuanzisha jamii mpya ya Binaadamu. Yesu alikuwa Adamu wa mwisho. Alikuja kama mzaliwa wa mwisho wa jamii ya adamu na mzaliwa wa kwanza wa jamii mpya.
Alipotundikwa msalabani alitundikwa pale kama Adamu wa mwisho mzaliwa wa mwisho wa jamii ya Adamu na aslili ya dhambi ya Adamu ilikufa.
Mungu aliweka uumbaji ulioanguka kifoni ndani ya Yesu na jamii ya Adamu ilikufa katika Kristo, Rumi 5:6
Mtu wa pili
Yesu akija kama mtu mpya wa mungu ambaye kwa hiyo jamii mpya ingeumbwa. Yesu alifufuliwa toka kwa wafu sio kama Adamu wa mwisho bali kama mtu wa pili kichwa cha uumbaji mpya, 1kor 15:22, 1kor 15:45-49.
Uumbaji mpya
Katika ubatizo katika maji tunatangaza kwa marafiki na wanao tufahamu wote kwamba sisi sote sio tena jamii ya Adamu na ufalme wagiza. Ni uumbaji mpya ndani ya Kristo, ni watu wa ufalme wa Mungu. 2kor 5:17, Efes 2:10
SOMO LA KUMI NA MOJA
ROHO MTAKATIFU
Baada ya yesu kufufuka toka wafu alionekana kwa wanafunzi wake kwa siku 40. Halafu walipokuwa wamekaa pamoja nae juu ya kilima kirefu alichukuliwa kwenda mbinguni mbele ya macho yao, mdo 1:1-11. Hata hivyo kabla hajaondoka Yesu aliwapa waliomwamini ahadi maalumu sana nay a ajabu, Yn 14:16-18, 16:5-7.
Yesu hakutuacha pekee yetu Duniani ametumwa roho mtakatifu kwetu.
ROHO MTAKATIFU NI MUNGU
Kitu cha kwanza kabisa ambacho lazima kukifahamu kuhusu roho mtakatifu ni kwamba roho mtakatifu ni mungu kweli. Mdo 5:3-4, kor 3:17.
Mungu amechagua kujidhihirisha yeye mwenyewe kwa Wanaadamu kama baba, mwana, roho mtakatifu. Hizi ni sura tatu tofauti za nafasi lakini bado hawa watatu ni mmoja.
KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU
Roho mtakatifu ni kipawa kwa ajili ya kila mwamini wakati mtu anapomwamini Yesu na kupokea wokovu. Yesu hutoa roho mtakatifu kuishi ndani ya mwamini ili kumgawia uzima wa kiroho, mdo 2:38-39, yohana 7:37-39
KAZI ZA ROHO MTAKATIFU
Katika maisha ya mwamini binafsi roho mtakatifu huja kuishi ndani ya mwamini na kumhudumia binafsi,
Anashuhudia kuhusu uhusiano wetu na mungu, rum 8:16, 1yoh3:24
Anafundisha, yoh 14:26
Anaongoza, rum 8:14 kwa kuwa wote wanaongozwa na roho wa Mungu hao ndio wana wa mungu
Anatusaidia kuishi maisha ya kumpendeza mungu, Gal 5:16, 17-25
Anatusaidia katika maombi, rum 8:26
Anatoa uzima kwa miili yetu, rumi 8:11
Yuko nsdani ya mwamini kwa ajili ya utumishi
Pamoja na kutoa roho mtakatifu kuishi ndani mwamini Mungu pia anataka kumjaza na kumkumbatia ilikumtia nguvu za kumtumikia na kumtukuza mungu duniani
Roho mtakatifu hutoa nguvu na ujasiri wa kushuhudia mdo 1:8, mdo 2:14-40
Huleta milki ya kiajabu 1kor 12:4, 8-10, mdo 2:4;10-46,19:6
Hushuhudiakwamba yesu yuhai mdo 5:30-32, 4:31-33
Huleta ufahamu mpya wa neno la mungu 1kor 2:9-10, yohana 16:13
Hujaza roho za watu ibada ya kweli ya mungu, Efeso 5:18-19, yohana 4:24
Humtukuza Yesu yoh 16:13-15, yoh 15:26
JINSI YA KUBATIZWA KQWA ROHO MTAKATIFU
Mungu anataka kwamba roho mtakatifu wake ambaye anakaa ndani yako kwasababu wewe ni mwamini wa yesu akujaze na kufurika kwa nguvu za kumtumikia yeye (Efeso 5:18)
Ni ahadi aliyo ahidiwa na mungu hivyo omba kwa ajili yake. Luk 11:13
Anza kumsifu mungu kadri unavyopokea kwa imani,. Luk 24:52-53
Unaweza kuzungumza kwa lugha ya kiajabu,. Mdo 19:6, mark 16:17, mdo 2:4,10:45-46, 1kor 14:5-18
